'Vacation walienda kufanya nini,' Mchekeshaji YY amfokea Jacque Maribe kwa kumwanika Eric Omondi

Muhtasari
  • Mchekeshaji YY amfokea Jacque Maribe kwa kumwanika Eric Omondi
  • Wakati huo huo dada yake Jacque alimshambulia Eric na kumpongeza dada yake kwa kumwanika Eric
yy
yy

Mchekeshaji Eric Omondi, na mwanahabari Jacque Maribe wamekuwa gumzo mitandaoni siku ya Jumanne, baada ya Jacque kumuanika Eric.

Kulingana na Jacque, Eric hajakuwa akiwajibikia mahitaji yake kama baba wa mtoto wao.

Mchekeshaji YY amezungumzia swala hilo, na kushindwa kwa nini Eric na mama wa mtoto wake walienda kujifurahisha pamoja kama Eric hakuwa ana wajibika.

"vacation walienda kufanya nini kama tangu mtoto azaliwe hakuna kitu mwanaume amemfanyia mtoto...alimsifia Eric mbele ya umma wakati huu..Walisifiana kwa posts...tofauti iko wapi?...wanawake ukisikia mwanamume hawajibiki na kuwavumilia kwa raha zako, unakuwa mshirika," Aliandika YY.

Eric amekejeliwa sana na wanamitandao, baada ya ukiri wake Jacque Maribe.

Wakati huo huo dada yake Jacque alimshambulia Eric na kumpongeza dada yake kwa kumwanika Eric.

"@Ericomondi sasa umefichulia,kumpigia dada yangu ukiwa kwenye mahojiano, ukifikira atacheza na wewe @jacquemaribe umemuanika kama nguo baridi kwa fence ya sengenge

Kazi mzuri mama,usimtumia mtoto wako kutafuta kikibaa ni ule analea si ule wa sperm donor.PS nangoja umalize kupark gari unitumie karo ya mtoto..lakini pole ulikuwa mwaka jana," Aliandika Cate.