logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jacque ni mama mbaya,'Eric Omondi hatimaye atoa sababu ya kufichua yale yamekuwa yakitendelea kati yake na Jacque Maribe

Pia anadai kuwa Maribe sio mama mzuri kwa mtoto wake kwa sababu hangeweza kufikiria kuhusu mtoto wake

image

Burudani03 November 2021 - 20:45

Muhtasari


  • Eric Omondi hatimaye atoa sababu ya kufichua yale yamekuwa yakitendelea kati yake na Jacque Maribe

Hatimaye Eric Omondi ametoa sababu ya kwa nini aliamua kumuweka wazi Jacque Maribe kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutuhumiwa kuwa hawajibikii mahitaji ya mwanawe.

Kulingana na Eric, Jacque Maribe alijibu kwenye picha yake na Miss P ambayo alikuwa ameiweka kwenye Instagram yake ambapo aliendelea na kutoa maoni akimshutumu Eric kwa kutowajibika.

Eric ameweka wazi kuwa hajahusika kikamilifu na maisha ya mtoto wao kwa sababu amekuwa akidai kupimwa DNA jambo ambalo Jackie amekuwa akipinga.

Akizungumza na Massawe Japanni ,Pia anadai kuwa wao wamekuwa wakipigana kwa faragha hadi pale JacqueMaribe alipoamua kuleta suala lao la faragha kwenye mitandao ya kijamii na kumfanya aonekane mbaya kwa Wakenya.

Eric anadai kuwa baada ya picha aliyopakia watu wengi walipiga hatua ya kumtafuta lakini  Maribe alitangulia kuandika aya inayomhusu badala ya kuwasiliana naye faragha ndiyo maana aliamua kuanika kile ambacho kimekuwa kikiendelea kati yao.

Pia anadai kuwa Maribe sio mama mzuri kwa mtoto wake kwa sababu hangeweza kufikiria kuhusu mtoto wake kabla ya kutangaza kila kitu kwenye mitandao ya kijamii.

"Baada yangu kupakia picha hiyo, watu wengi walinipigia simu na kuniuliza nini haswa kinaendelea, ilhali Jacque alimua kuenda mitandaoni na kuanika kila kitu

Naweza kusema kwamba Jacque sio mama mzuri kwa mtoto wake, kwani hakufikiria kuhusu mwanawe alipoanika kila kitu," Asema Eric.

Pia amezungumzia kuwa amewahi fanya DNA ilhali Jacque hakuwa jambo ambalo hangekubalishwa kwani sio halali kama mama mtoto hayuko.

Hii hapa audio ya mazungumzo yao;

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved