"Sijateuliwa katika tuzo yoyote," Harmonize akanusha tuzo za AEAUSA ambazo alikuwa ameteuliwa

Muhtasari
  • Harmonize akanusha tuzo za AEAUSA ambazo alikuwa ameteuliwa
  • Kitu ambacho alikihisi licha ya kazi kubwa anayofanya, bado hakizai matunda linapokuja suala la Tuzo alizonazo
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Siku chache zilizopita, Harmonize alikuwaana vuma mitandaoni baada ya kunaswa akilalamika kuwa hawi akiteuliwa kwenye tuzo tofauti kama wasanii wenzake wanavyofanya.

Kitu ambacho alikihisi licha ya kazi kubwa anayofanya, bado hakizai matunda linapokuja suala la Tuzo alizonazo.

Harmonize hata hivyo aliandika kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram na kuwaonya mashabiki wake waaminifu wa Kondegang FC kutompigia kura katika Tuzo ambazo alikuwa ameteuliwa.

Ambapo aliandika akisema,

"Sijateuliwa katika tuzo yoyote, kwa hivyo tafadhali usipoteze kifurushi chako cha Kondegang FC pekee. "

Ujumbe ambao umevuta hisia za mashabiki wake wengi, ambao wanajiuliza nini kinaweza kuwa sababu ya kukataa uteuzi huo.

Tuzo za hivi punde zaidi zilikuwa tuzo za AEUSA ambapo aliteuliwa katika vipengele tofauti kama vile msanii bora wa kiume wa mwaka.

Swali kuu ambalo limesalia akilini mwa mashabiki kuna ni?