Google yasheherekea siku ya kuzaliwa ya mwanzilishi wa masomo ya lugha za ishara barani Afrika

Muhtasari

•Profesa Okoth Okombo, ambaye ametoa zaidi ya machapisho 30 kuhusu Muundo na misamiati ya lugha za watu wasiosikia (Viziwi), anatajwa kama mwanzilishi wa masomo ya lugha za ishara barani Afrika.

Image: GOOGLE

Tovuti ya google leo imeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa na kutimiza miaka 71 ya alieyekuwa profesa na mwandishi mashuhuri nchini Kenya Okoth Okombo kwa kuweka picha yake kama nembo katika ukurasa wa mbele wa google (Doodle)

Profesa Okoth Okombo, ambaye ametoa zaidi ya machapisho 30 kuhusu Muundo na misamiati ya lugha za watu wasiosikia (Viziwi), anatajwa kama mwanzilishi wa masomo ya lugha za ishara barani Afrika.

Katika maisha yake Okombo, alifanya kazi kwa bidi ili kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu wa kusikia (Viziwi) na anatambuliwa kimataifa kama mmoja wa viongozi wasomi wa lugha ya ishara duniani.

Okombo alifanya utafiti kuhusu lugha ya ishara kenya (Kenyan Sign Language) mwaka 1991, Utafiti uliosababisha kupitishwa kwa matumizi ya lugha ya ishara nchini Kenya na kuruhusu jumuiya ya viziwi kupata fursa mpya katika jamii.

Kwa mafanikio yake, Shirikisho la viziwi ulimwenguni (World Federation of the Deaf) lilimchagua Okombo kuwa rais wa shirikisho hilo kimataifa kuanzia mwaka 1992 hadi 1995.

Msanii wa Kenya Joe Impressions ndiye aliyepata fursa ya kuchora picha hiyo anasema alifurahishwa kufanya kazi ya kuchora nembo hiyo ya Okombo iliyotumika katika ukurasa wa mbele wa kutafuta wa google

“Baada ya kufanya utafiti mtandaoni, nikafiria kuwa ni lazima nimuoneshe Profesa akifanya kile kilichomuunganisha na wanafunzi wake wengi zaidi na hicho ni kufundisha, nilitaka kupata kitendo muhimu ambacho unaweza kupata wakati wa kufundisha” alisema Impressions.

Okombo alifariki November 1mwaka 2017, katika Hospitali ya Aga Khan Hospital iliyopo Nairobi, Kenya alipokuwa akipatiwa matibabu.