Ninajivunia,kwa umbali nimetoka,'Nadia Mukami asema anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Ushauri wake Nadia MUkami kwa wasichana anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa
Nadia Mukami
Image: INSTAGRAM

Nadia Mukami ni mmoja wapo wa wanamuziki anayependwa zaidi na watu wengi kwa ajili ya bidii ya kazi yake.

Sauti za Nadia kwa kawaida hufanya vizuri na hii huacha maonyesho yake mengi yakivuma sana mitandaoni, na nyimbo zake kupokea watazamaji zaidi ya milioni moja kwenye youtube.

Nadia ni mhitimu wa hivi majuzi wa Chuo Kikuu cha Maseno ambapo Nadia Alisomea Digrii ya akaunti za Fedha.

Hata hivyo mapenzi ya Nadia kwa muziki hayangemruhusu kuangazia kazi yake ya kifedha. Nadia alichagua Muziki.

Tasnia ya muziki inaonekana kumkaribisha Nadia kwa mikono miwili kwani Nadia anafanya vyema akiwa kwenye tasnia ya muziki.

Nyimbo nyingi za Nadia ni nyimbo maarufu. Nadia amebahatika kushirikiana na  baadhi ya wasanii wa kustaajabisha na nyimbo pia zinafanya vizuri sana.

Nadia amewaahidi mashabiki wake maonyesho mazuri katika siku yake kuu kama njia ya kuwathamini mashabiki wake wa ajabu.

Pia huku ajiandikia ujumbe wa heri njema wa siku yake ya kuzaliwa amewashauri wasichana wadogo ambao wanaona ndoto zao hazitawahi timia.

Pia msanii huyo amesema kwamba anajivunia sana, na umbali ambao ametoka;

"HERI  NJEMA YA SIKU YA 25 YA KUZALIWA KWANGU!!!! 🎂 PICHA YA 5 ITAKUSHTUA🤣😂😂😂 IMENISHTUA PIA!!!

Kusema kweli, ninajivunia mwenyewe na umbali niliofika na nataka kumwambia kila msichana mdogo kijijini, unaweza kufuata ndoto zako na kuzifanya kuwa kweli!!!!!

Ulikotoka haifafanui unaenda wapi! Mimi ndiye muumini mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii na kubadilisha hadithi yangu ambayo watoto wangu watajivunia mimi💙

KWA kila mtu ambaye amechangia safari yangu, wewe ndio sababu ya mimi kuwa Mwana PopStar wa Kiafrika!!! nakushukuru! Kila kampuni, mtangazaji wa klabu, mtangazaji wa hafla, mtunzi wa mitandao ya kijamii, msanii mwenzangu katika kolabo na shabiki ambaye ametiririsha muziki wangu!

Wewe ni Shujaa wangu na sehemu ya kubadilisha historia yangu!!! Safari bado ndio tunaaanza 🙏 ( Picha za kuomba misaada food hizi sasa) 🤣," Aliandika Nadia.

Heri njema siku yako ya kuzaliwa Nadia kutoka kwetu wanajambo.