Haya yote yatapita,'Nana Owiti amwambia Michelle Ntalami

Muhtasari
  • MKewe King Kaka amshauri Michelle Ntalami kwa yale anapitia
  • Nana alimtumia Ntalami ujumbe, huku akimwambia kwamba hayo yote yatapita

Mtangazaji maarufu wa runinga nchini Kenya, Nana Owiti ametuma ujumbe kwa mjasiriamali, Michelle Ntalami baada ya kufunguka na kushiriki kilichosababisha kutengana kwake na Makena.

Nana aliweka picha ya Michelle kwenye mitandao yake ya kijamii na upande wa kulia alituma ujumbe kwa mfanyabiashara huyo maarufu.

Ntalamikupitia kwenye  mitandao yake ya kijamii akifichulia umma kuwa aliachana na mpenzi wake wa muda mrefu Makena.

Mwanamke huyo mfanyabiashara alishiriki chapisho hilo refu akiwapa wafuasi wake maelezo yote kuhusu kilichosababisha kuachana kwao.

Nana alimtumia Ntalami ujumbe, huku akimwambia kwamba hayo yote yatapita.

Nana alimwambia Michelle kwamba:

'Kisichomuua kitamfanya awe na nguvu zaidi'. Nana alisema kuwa mjasiriamali huyo asiwe na wasiwasi kwani haya yote yatapita.

Owiti alimhimiza Ntalami kuendelea kusonga mbele na asiwe na wasiwasi kuhusu yaliyopita.

"Haya yote pia yatapita malkia," Nana alimwandikia Michelle.

Chapisho la Nana lilizua hisia kutoka kwa wanamitandao. Wengi walitoa maoni yao kwa kusema kwamba Nana ni rafiki mzuri.