Shetani hukutaka nishuhudie siku hii,'Size 8, DJ Mo washerehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wao

Muhtasari
  • Size 8, DJ Mo washerehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wao
Muraya-ladasha-size-8-mpasho
Muraya-ladasha-size-8-mpasho

Hakuna kitu kinachokufanya uwe na hisia kama kukumbuka baadhi ya matukio yako machafu ya maisha.

Hii itakufanya ujisikie chini, mwenye furaha na mnyenyekevu mbele za Mungu kwa wakati mmoja.

Kufuatia kile kilichotokea kwa Size 8 miezi michache iliyopita, kwa hivyo ameelezea haya yote.

Leo ni siku ya kuzaliwa ya mtoto wake@Murayajuniour na ametumia ukurasa wake wa Instagram kushiriki furaha yake na mashabiki wake ambao wameungana naye kumsifu Mungu.

Alitaja kuwa kufikia sasa angekuwa amekufa na hangeshuhudia siku hiii ya pekee.

Size 8 alipoteza mtoto wakati wa operesheni hivi majuzi ambayo karibu apoteze maisha yake.

"Muujiza mdogo wangu @muraya.jnr anatimiza miaka miwili leo uuuuuuuwwwiii siwezi kutulia huu ni muujiza mkubwa hatua kubwa...... Woi shetani hakutaka nishuhudie siku hii ulitaka kuniua lakini ona ukuu wa Mungu wangu niko hai kuona jrn akitimiza miaka 2uuuuwwwiiii ebu tunaimba wimbo wa Yesu wa sherehe wa @evelynwanjiru_a uuuuwwwiiii muone Mungu. Happy birthday @muraya.jnr, @djmokenya swity muone Mungu uuuuwwwiiii cc @ladashabelle.wambo," Aliandika Size 8.

DJ Mo kwa upande mwingine amesimama naye wakati huu wote. Pia amechapisha picha za utoto za mtoto wake akimtakia kila la heri maishani.

"Wewe ni shuhuda, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili yako .. imekuwa ni safari lakini wewe ni simba 🦁. . siku kama leo ulikuja duniani na hapa tunasherehekea mwaka wako wa pili. 🎉🎁 Heri ya siku ya kuzaliwa @muraya.jnr … Mungu amekuwa mwaminifu. HERI 2 JNR. Baba yuko kazini.. hivi karibuni tutakuona. Nisaidie kumtakia SIKU NJEMA mwanangu 🎁🎈🎂🎊🎉."