'Nilipatwa na msongo wa mawazo,'Mwanasosholaiti Shakilla aeleza sababu ya kutokuwa mitandaoni

Muhtasari
  • Kulingana na mwansosholaiti huyo, alichukua mapumziko kutoka kwa mitandao ya kijamii kutokana na shinikizo ya watu walio kwenye mitandao
Shakilla
Image: INSTAGRAM

Shakilla kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ametoa sababu ya kutokuwa mitandaoni kwa muda sasa, kama alivyokuwa baada ya kufahamika sana mwaka jana.

Kulingana na mwansosholaiti huyo, alichukua mapumziko kutoka kwa mitandao ya kijamii kutokana na shinikizo ya watu walio kwenye mitandao.

Shakilla aliendelea kufichua kwamba alihisi kama alikuwa amekwama katika maisha kama watu wengine walikuwa wakiendelea mbele.

Aidha alisema kwamba alihisi kwamba mitandao ya kijamii haikuwa mahali pema pa afya yake.

Yote tisa kumi ni kuwa alidai kwamba alikuwa amepatwa na msongo wa mawazo alipokuwa akiingia kwenye mitandao ya kijamii.

Huu hapa ujumbe wake;

"Nilichukua mapumziko kutoka kwa mitandao ya kijamii kwani nilikuwa napatwa na msongo wa mawazo nilipokuwa nikiingia kwenye hizi mitandao

Mitandao ya kijamii itakufanya ufikirie kwamba umekwama maishani, hauendi mbele,haikuwa nzuri kwa afya yangu kusema ukweli

Ukiwatazama watu wakiwa kwenye viwango vingine maishani, na kulinganisha na viwango vyetu, hiyo sio afya njema," Alisema Shakilla.