'Niko sawa,'Muigizaji Nyce Wanjeri hatimaye azungumza baada ya uvumi kuwa anakabiliana na vurugu za nyumbani

Muhtasari
  • Muigizaji Nyce Wanjeri hatimaye azungumza baada ya uvumi kuwa anakabiliana na vurugu za nyumbani
Nyce Njeri
Nyce Njeri

Muigizaji Nyce Wanjeri hatimaye amezungumza baada ya uvumi kwamba alikuwa akikabiliwa na unyanyasaji wa nyumbani kuibuka mtandaoni.

Uvumi huo ulizuka baada ya mwanamitandao  wa Facebook kuona alama za mikwaruzo kwenye shingo na uso wake aliposhiriki mchezo mfupi  kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Nyce alimwambia mwanablogu Edgar Obare kwamba yuko sawa na hakabiliwi na vurugu za aina yoyote maishani mwake.

Alisema kuwa alikuwa amerekodi mchezo huo baada ya kucheza jukumu la kupigana kwenye kipindi anachoigiza kwenye runinga ya Inooro.

"Haya Edgar, ningependa kufafanua kuwa mimi ni mzima na sijakumbana na vurugu zozote maishani mwangu. Huo ulikuwa mchezo ambao nilifanya  baada ya kuigiza kipindi ambacho huwa naigiza. kwenye runinga ya Inooro. Niko sawa. Jukumu niliokuwa nikicheza lilikuwa jukumu la kupigana. Salamu za fadhili" Aliandika.

Nyce alifahamika sana baada ya kuigiza kwenye kipindi cha Auntie Boss, huku akizidi kuigiza kwenye vipindi mbalimbali na kupata umaarufu mkubwa.