'Tafadhali jina langu lisitajwe,'King Kaka amwambia Eric Omondi

Muhtasari
  • King Kaka amwambia Eric asitaje jina lake kwenye drama yake na wasanii
King Kaka
Image: Hisani

Vita kati ya mchekeshaji Eric Omondi, na wasanii wa humu nchinii zimezidi kugonga vichwa vya habari mitandaoni.

Eric amekuwa akiwashambulia wasanii na kuwaambia kwamba wamelala.

Baada ya madai yake, wasanii kadhaa walijitokeza na kumjibu Eric Omondi, huku mmoja wao aiwa ni msanii Bien ambaye alimuonya Eric amkome.

Akiwa kwenye mahojiano wikendi Eric alisema kwamba;

"Wao ni wa wastani na wanachofanya ni kuninyanyasa tu. Tutawatoa kutoka Bien hadi kwa King Kaka."

Rapa King Kaka hakupendezwa na maelezo hayo ya jumla, huku akimjibu Eric na kumwambia kwamba anamuombea apate amani.

King Kaka alisema, "Sijui unapitia nini lakini tafadhali jina langu lisitajwe. Naomba upate amani unayo nambari yangu unaweza kuwasiliana nayo kila wakati."

Eric alijibu kwa kusema,

"@thekingkaka ndugu yangu siyuko sawa.sina amani kwani tangu utoe kibao cha  DUNDAIING hujatoa ngoma ingine competitive yenye inaeza kuchezwa inje ya Kenya

Bro, mimi pamoja na Wakenya wengi tumesikitishwa na hali ya kusikitisha ya sekta yako, hakuna tofauti tofauti na maji taka," Alisema Eric.