'Eric Omondi lazima aachiliwe,'Msanii KRG akashifu kukamatwa kwa mchekeshaji Eric

Muhtasari
  • Mchekeshaji  Eric Omondi anadaiwa kuzuiliwa katika kituo cha polisi baada ya kukamatwa alipokuwa anaongoza maandamano jijini Nairobi
Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Mchekeshaji  Eric Omondi anadaiwa kuzuiliwa katika kituo cha polisi baada ya kukamatwa alipokuwa anaongoza maandamano jijini Nairobi.

Msanii huyo asiyepungukiwa na drama anaripotiwa kutiwa mbaroni asubuhi ya Jumanne alipokuwa ameongoza kikundi cha vijana kuandamana nje ya bunge la kitaifa kurekebisha sekta ya muziki nchini.

Eric alikuwa ametoa wito kwa wasanii na waandishi wa habari washirikiane naye katika maandamano kuelekea bungeni kudai kuchezwa zaidi kwa sanaa ya Kenya na malipo bora kwa wasanii wakati wa tamasha.

Mchekeshaji huyo ambaye amekuwa akivuma sana hivi karibuni anadai vituo vya burudani vicheze asilimia 75 ya muziki wa Kenya.

Kwenye video ambayo imeenezwa sana mitandaoni mchekeshaji huyo anaonekana akikokotwa na polisi akielekezwa kwenye gari lililokuwa limesubiri kumpeleka kituoni.

OCPD wa kituo cha Central Adamson Bungei amesema Omondi alikamatwa kwa kusababisha fujo nje ya bunge.

"Hakuwa amefuata taratibu za kufanya maandamano. Hata hivyo tunampanga,” Bungei amesema.

Rappa KRG kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amekashifu kukamatwa kwa Eric huku akisema kwamba alikuwa anapigania wasanii.

"Nimeona kile kimetendeka jijini Nairobi,Eric amekamatwa anapigania wasanii na sijaona msanii yeyote huko

Mimi walisema kuwa ni msanii chipukizi, naenda kumuangalia na ndani ya masaa mawili lazima akue ameachiliwa, hakuna vile Eric atatiwa mbaroni kwa ajili ya wasanii ambao hawafanyi chochote," KRG Amesema.

Ujumbe wake KRG uliibua gumzo, na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

wanjikustephens: Anapigania wasanii ama anapiga wasanii🤷🏾‍♀️🤷🏾‍♀️🤷🏾‍♀️

nixsz8Wazanii: amkeni twende town tufungue erick big up the don krg🔥🔥

ownesnzeki: Wewe Tu ndio msanii umesimama na Eric👏👏👏big up bro

rickii55: Beast mode activated...your the real artist here in Kenya... The rest hatuwatambui sasa...Ata OG mwenyewe