Makubwa:Mpenzi wangu aliniambia yeye ni msagaji-Mwanamume afichua

Muhtasari
  • Kama huyajaona basi yapo njiani .ndio msemo pekee ambao sasa utakuacha na taswiraya mambo ya kutisha na hata kushangaza katika karne hii

Kama huyajaona basi yapo njiani .ndio msemo pekee ambao sasa utakuacha na taswiraya mambo ya kutisha na hata kushangaza katika karne hii.

Eric  alimchumbia Essie kwa muda na badala ya kuangazia masuala ya uhusiano wake ameanza kutafakari iwapo kwa kweli alifanya kosa kuchumbiwa na mwanamume …kisa na maana?

Kwa sababu maajuzi amegundua kwamba huenda yeye ni mpenzi wa jinsia moja ama  huenda yeye ni mtu wa kujihusisha katika mapenzi na jinsia zote mbili .

Hajui lakini ni mojawapo kati ya hizo .

  Sasa kuna haki kwa kila mtu kufanya anachotaka na  maisha yake ya kimapenzi ,lakini haya ya Essie sasa yanashangaza kwa sababu  anasema yeye anampenda dadake mpenzi wake yaani shemeji yake.

Kwa ujasiri mkubwa Essie alimwambia Eric kwamba yeye ni msagaji na hamna kitu ambacho anaweza fanya.

"Mwaka mmoja baada ya kuwa kwenye uhusiano alikuwa na ujasiri  wa kuamka siku moja na kuniambia i don't do men anymore, na kuniambia kwamba hajakuwa na hisia zozote zangu na sikuwa namtimizia haja yake

Nilijua hawa 'daughters of jezebel' hawajui mapenzi ni nini, nilikuwa nimeona mwenzi wangu wa maisha lakini kile sielewi aligundua lini kamba yeye ni msagaji

Aliniambia kwamba anampenda dada yangu, niko kwenye dilema sijui nifanyeje inauma lakini itabidi nimuachilie aende."