Naamini sana katika mapenzi, nina watoto 4 na baby mama 3-KRG afunguka kuhusu maisha yake

Muhtasari
  • Rappa KRGte Don amekuwa akivuma mitandaoni baada ya kutangaza kwamba anampa mkewe talaka
  • Kulingana na KRG, mkewe aliwasikiza watu wa nje badala ya kujenga familia yake
KRG
Image: Hisani

Rappa KRGte Don amekuwa akivuma mitandaoni baada ya kutangaza kwamba anampa mkewe talaka.

Kulingana na KRG, mkewe aliwasikiza watu wa nje badala ya kujenga familia yake.

Akiwa kwenye mahojiano  na mseto East Africa alifichua kwamba mkewe hakumtambua pamoja na wanawe, ila alitambua  familia yake na ndugu zake.

"Mwanamke ni kama nguzo ya familia na akipotea haya basi familia inatawanyika, lakini kila mtu anamaamuzi yake lakini mimi na watoto wangu tushaazoea

Watoto wangu wanajua kila kitu,lakini tuache hayo kwa maana ana maisha yake na mimi nina maisha yangu

Kiini kikubwa cha ndoa yangu kuvunjika aliwasikiza watu wa nje, hatutambua mimi na watoto wangu  kama familia yake aliamini upande wao na kuwasikiza

Uhusiano wangu na Mungu ni mzuri, kwa maana Mungu huwa anakuja kwanza familia alafu pesa," Alisema KRG.

Pia msanii huyo alisema kwamba hajawahi mdanganya mke wake, kwani akiwa kwenye uhusiano na mwanamke mwingine alikuwa ameshaamwambia.

Aidha alifichua ana watoto 4 na baby mama 3.

"Mimi nina watoto 4 na baby mama 3, mtoto wa kwanza nilipata nikiwa na miaka 19, na sikuwa tayari kuchukua majukumu lakini huwa namsaidia na kuwajibika kama baba yake

Mke ambaye aliniacha nilikuwa nishaa muoa kitamaduni,pia alikuwa anafahamu kwamba nina mtoto na mwanamke mwingine

Sijawahi mdanganya katika ndoa, nimeona mambo mengi lakini sijawahi ona mwanamke na waume wawili."