Nilipoolewa nilikuwa na msongo wa mawazo-Msanii Mercy Masika

Muhtasari
  • Mwimbaji wa nyimbo za Injili Mercy Masika anasema kujisalimisha katika ndoa yako hakumfanyi mwanamke kuwa mdogo katika ndoa
82165159_619911565463731_8777097389591686827_n(1)
82165159_619911565463731_8777097389591686827_n(1)

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Mercy Masika anasema kujisalimisha katika ndoa yako hakumfanyi mwanamke kuwa mdogo katika ndoa.

Katika chapisho la kwenye ukurasa wake wa instagram, Masika alisema kujisalimisha kunasaidia ndoa kustawi katika njia ya Mungu.

Aliongeza kuwa alipoolewa, alikuwwa na msongo wa mawazo na  hakuwa mtiifu hadi alipojifunza kuwa hekima ya Mungu ni bora kuliko yake.

"Kujitiisha kwa mumeo hakukupunguzii. Inasaidia ndoa yako kuifanya kwa njia ya Mungu," aliandika Mercy Masika.

Pia aliwashauri wanawake kuwa kujisalimisha wa waume zao sio uonevu bali ni heshima.

"Nilipoolewa nilikuwa na msongo wa mawazo, nilihuzunishwa na maneno hayo. Nilikuwa kama neeveeer. Hadi nilipojifunza hekima ya Mungu ni bora kuliko yangu.

Kujisalimisha sio uonevu..ni Kumheshimu mumeo... ni kumtendea kwa heshima nimepata manufaa ya kujisalimisha katika ndoa hivi kwamba nilijifunza kuwa nina uwezo mkubwa sana ninapojitolea."

Ujumbe wake uliwavutia wanamitandao na hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

celestinedonkormusic: Absolutely true

princessjackey: I won't stone you😂😂😂 you just spoke a bitter truth😂😂😂catch you on the YouTube😍

steny_nyawira: On the same note, submission is only applicable where both people are godly and have submitted to god the father

paul__mbithi: This is so wonderful. I wish many could read & understand your mind