Kama hujapatana na Akothee hujapatana na malaika-Mpenziwe Akothee Nelly Oaks asema

Muhtasari
  • Mama huyo wa watoto watano amelazwa katika wadi ya wagonjwa maarafu katika hospitali moja nchini
  • Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee ameonyesha hali ya kifahari ya chumba alicholazwa huku akionekana akihudumiwa na wauguzi maalum
Nelly Oaks na Akothee
Nelly Oaks na Akothee
Image: INSTAGRAM//NELLY OAKS

Mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri nchini Esther Akoth almaarufu kama Akothee angali anaendelea kupokea matibabu hospitalini ambako alilazwa mwishoni mwa wiki iliyopita kufuatia maradhi yasiyotambulishwa.

Mama huyo wa watoto watano amelazwa katika wadi ya wagonjwa maarafu katika hospitali moja nchini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee ameonyesha hali ya kifahari ya chumba alicholazwa huku akionekana akihudumiwa na wauguzi maalum.

Siku ya Jumanne, Oaks alitumia akaunti yake ya Instagram kummiminia Akothee sifa, akikumbuka jinsi kila mara anapigania wengine kuwa na maisha bora.

"Huyu ni mwanamke mmoja ambaye amekuwa kila wakati kwa kila mtu na kila mtu, anajitokeza na haachi chochote kujaribu kuifanya dunia kuwa mahali pazuri. Wakati wowote ninapomwona ameshuka, najua ni wakati huo nguvu zake zitaisha. Hebu sote tujifunze kumthamini Esther Akoth Kokeyo.

Kama hujakutana na Esther, bado hujaonana na Malaika. Sote tumshukuru na kumshukuru Mungu kwa kutuleta Esta katika maisha yetu. Nakupenda Esther @akotheekenya,” aliandika Nelly Oaks.