Asanteni kwa maombi yenu,'Akothee awashukuru mashabiki baada ya kutoka hospitalini

Muhtasari
  • Akothee ni mwanamke mchapakazi ambaye hufanya juhudi zote kuhakikisha kwamba anaipatia familia yake mahitaji bila kutegemea yeyote kama mama 'single mother
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Akothee ni mwanamke mchapakazi ambaye hufanya juhudi zote kuhakikisha kwamba anaipatia familia yake mahitaji bila kutegemea yeyote kama mama 'single mother.'

Amekuwa mgonjwa kwa takribani wiki mbili sasa na kwa neema za Bwana ameruhusiwa kutoka hospitalini na marafiki, familia, ndugu na watoto wake wamefurahi kumuona akiwa na nguvu tena.

Kwenye chapisho hilo, aliandika maandishi "home sweet home, asanteni nyote kwa maombi yenu" ambayo ina maana kwamba kwa sasa yuko nyumbani kwake na anawashukuru wale wote ambao wamekuwa na bidii ya kumjulia hali na kumuombea.

Pia alimshukuru mpenzi waeke Nelly Oaks kwa kuwa naye, pia aliwashukuru watoto wake ambao wamekuwa wakijulia hali kila wakati.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alimshukuru sana mpenzi wake kwa kuwa naye, huku akimhakikishia kwamba atamzalia watoto 2.

"Nakusherehekea mfalme wangu @nellyoaks hakuna mwanaume anayeweza kunistahimili kwani wengi wao wanamfuata AKOTHEE & sio Esther Akoth Kokeyo , haufuati chochote ila ustawi wangu

Ninakutangaza wewe shujaa wangu, mpenzi wangu, mpenzi wangu, mlinzi wangu na Malaika mlezi wangu! NELSON OYUGI, watoto wawili kwa ajili yako kutoka tumboni mwangu,na hakuna mtu anayeweza kuniambia masihara isipokuwa wanaweza kulipa bili zangu hata kwa siku moja tu." Alisema Akothee.