Ushateka huyu?Wanamitandao watoa hisia tofauti baada ya Willy Paul kumsajili msanii wa kike

Muhtasari
  • Mwanamuziki Wilson Ouma Opondo almaarufu Willy Paul amemsajili msanii mwingine wa kike, miezi kadhaa baada ya kuondoka kwa mwanamuziki wake wa kwanza Miss P
Pozze 1
Pozze 1

Mwanamuziki Wilson Ouma Opondo almaarufu Willy Paul amemsajili msanii mwingine wa kike, miezi kadhaa baada ya kuondoka kwa mwanamuziki wake wa kwanza kusajili Miss P.

Siku ya Alhamisi, Pozze, alizamia mitandao ya kijamii kumkaribisha msanii mpya anaye tambulika kama Queen P kwenye Lebo yake ya Saldido International.

β€œSiku zote ni muhimu kuweka heshima mbele na tamaa nyuma. Kwani ni vigumu sana kwenda mbali bila heshima.. Watu hawapendi kuona wengine wakiendelea kwa hivo kuwa makini sana na unaempa sikio.

Hata hivyo, nisaidie kumkaribisha msanii mpya wa kike wa @saldido_international. @queenp254 tumekuchagua kwa sababu unastahili nafasi hiyo. Mungu akuongoze katika safari hii.. uwe makini sana unajihusisha na nani hasa hawa wachekeshaji.. wana vichekesho vingi sana πŸ˜† 🀣 πŸ˜‚ Karibu nyumbani.. @saldido_international hits only. Siwezi kungoja ulimwengu kusikia kile ulichonacho,” aliandika Willy Paul.

Usajili wa Queen P unakuja miezi kadhaa baada ya msanii wake wa kwanza Miss P kudai kuwa alinyanyaswa kingono na bosi wake wa zamani.

Walakini, mnamo Novemba 12, Pozze alishiriki hati za korti zilizomtaka Mtangazaji Ali kufuta mahojiano na Miss P ambaye alidai kwamba mwimbaji huyo alimnyanyasa kingono mara kadhaa.

Nyaraka za mahakama za tarehe 12 Novemba 2021 zilienda mbali zaidi kueleza kuwa yeyote anayeeneza/kusambaza video hiyo anaweza kushtakiwa katika mahakama ya sheria kwa kukashifu.

Wanamitandao walitoa hisia tofauti na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

_had.id_: MkunajiπŸ˜‚ushateka huyu

obby_visuals: πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘mali safi.....usimtekenyeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

jaredpozze: Congratulations Mr. Pozze πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ‘πŸ‘

iam.delvin._vuguza: Haiya after some few month tutaskia l fell in love with willypaulπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚then he forced me blabla blaπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œloading πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

kenn.edy9022: πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯tunangoja sana tuone vyenye ako

shanks_4870: Waiting for her projects , hope for the bestπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯