Davido kutoa msaada wa Sh68M kwa mayatima baada ya kuchangiwa pesa na mashabiki

Muhtasari

•Mapema wiki hii, mwanamuziki huyo maarufu aliwaomba mashabiki wanaoamini kuwa "Aliwapa wimbo mzuri" kumtumia pesa kwenye akaunti ya benki iliyokuwa na majina yake.

•Pesa zitakazotolewa mayatima ni pamoja na msaada uliotolewa na mashabiki pamoja na mchango binafsi wa naira milioni 50.

Image: INSTAGRAM// DAVIDO

Nyota wa muziki miondoko ya Afrobeats Davido anasema atatoa naira milioni 250 ($608,000; £450,000)  (Ksh 68, 000,00) kwa mayatima nchini Nigeria baada ya mashabiki wake kumtumia pesa.

Mapema wiki hii, mwanamuziki huyo maarufu aliwaomba mashabiki wanaoamini kuwa "Aliwapa wimbo mzuri" kumtumia pesa kwenye akaunti ya benki iliyokuwa na majina yake.

Jumamosi Davido amesema kuwa ombi hilo lilikuwa "la mzaha", lakini limepita kiwango cha matarajio yake.

Aliwashukuru wote waliompa msaada wa pesa, wakati alipokuwa akitangaza jinsi zitakavyotumiwa.

Pesa zitakazotolewa mayatima ni pamoja na msaada uliotolewa na mashabiki pamoja na mchango binafsi wa naira milioni 50.

Davido anachukuliwa kama nyota mkubwa zaidi wa muziki barani . Alishijnda tuzo za muziki za MTV na BET na kushirikiana kimuziki na wasanii wa kimataifa akiwemo Chris Brown na Nicki Minaj.

Ombi lake kupitia mitandao ya kijamii lilipokelewa kwa mitazamo tofauti. Baadhi walisema kuwa nyota huyo, ambaye anawafuasi zaidi ya milioni 22 katika Instagram, mara nyingi huonyesha maisha yake ya kifahari kwenye mtandao.

Katika ujumbe mmoja wa Twitter uliokuwa na emoji jza vicheko, Davido alisema lengo lake ni kuchangisha pesa ili kuwezesha gari lake la kifahariaina ya Rolls-Royce kuruhusiwa kuondoka bandarini.

Halafu alitoa maelezo ya akaunti na picha ya simu inayoonyesha garama ya gari hivyo inavyozidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda kutokana na kuchelewa bandarini.

Katika taarifa yake ya Jumamosi, muimbaji huyo amesema lilikuwa ni lengo lake kuchangisha pesa kwa ajili ya siku ya kuzaliwa kila mwaka ili kutoa msaada kwa jamii.

"Kila mara nimekuwa nikipenda sana kurudisha mkono na kuwasaidia watu," alisema.