"Kumbukeni Diana Marua katika maombi yenu!" Bahati afichua mkewe amelazwa hospitalini

Muhtasari

•Bahati ametangaza kuwa mpenzi wake anaendelea kupokea matibabu hospitalini baada ya kushambuliwa na maradhi yasiyothibitishwa siku ya Jumapili.

•Ameambatanisha ujumbe wake na picha za Diana akiwa amelala kwenye kitanda cha hospitali huku akiwa na sindano iliyofungwa mkononi.

Image: INSTAGRAM// BAHATI

Mwanamuziki wa nyimbo za injili na za mapenzi Kelvin Kioko almaarufu kama Bahati ametoa wito kwa mashabiki wake waombee mkewe, Diana Marua afueni ya haraka.

Bahati ametumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza kuwa mpenzi wake anaendelea kupokea matibabu katika kituo cha afya cha Komarock baada ya kushambuliwa na maradhi yasiyothibitishwa siku ya Jumapili.

Baba huyo wa watoto wanne amesema usiku wa kuamkia Jumatatu umekuwa mgumu sana kwa familia yake baada ya nguzo ya boma kulazimika kulala hospitalini.

"Jana Ulikuwa Usiku Mrefu kwa Familia Yetu. Mke Wangu aliugua na kuishia kulazwa 😭 Muweke @diana_marua katika Maombi yenu" Bahati ametangaza.

Ameambatanisha ujumbe wake na picha za Diana akiwa amelala kwenye kitanda cha hospitali huku akiwa na sindano iliyofungwa mkononi.

Mamia ya mashabiki wamejumuika chini ya chapisho la Bahati kuonyesha upendo na kumtakia malkia huyo afueni ya haraka.

@kabusimon: @diana_marua upone katika jina la Yesu

@mainawakageni Poleni

@ambussi_ Atapona katika jina la Mungu

@_etern_ upone haraka