Msanii wa nyimbo za injili Ruth Matete amkumbuka mumewe huku kuadhimisha siku yao ya harusi

Muhtasari
  • Ni furaha ya kila mwwanamke na mwanamume, kuishi kwenye ndoa baada ya kufunga pingu za maisha
  • Lakini mambo hayakuwa vile kwa mwanamuziki Ruth Matete kwani alimpoteza mumewe miezi mitano baada ya kufunga pingu za maisha
ruthmatete
ruthmatete

Ni furaha ya kila mwwanamke na mwanamume, kuishi kwenye ndoa baada ya kufunga pingu za maisha.

Lakini mambo hayakuwa vile kwa mwanamuziki Ruth Matete kwani alimpoteza mumewe miezi mitano baada ya kufunga pingu za maisha.

Mume wa marehemu Ruth Matete kwa bahati mbaya aliaga dunia tarehe 12 Aprili 2020, na hii ilikuwa miezi 5 tu baada ya wenzi hao kufunga ndoa.

Na kuhusu kilichosababisha kifo chake,  alikufa kutokana na kushindwa kwa viungo vingi baada ya kuungua kwa asilimia 60 kutokana na ajali ya kulipuka kwa mtungi wa gesi.

KUpitia kwenye ukurasa wake wa instagram Ruth, aliadhimisha miaka 2, November 22, na kusema kuwa;

"Kama Baba Toluwa angekuwa hapa leo, tungekuwa tunasherehekea kuadhimisha miaka 2 katika ndoa yetu. Lakini hata sasa Mungu bado ni mwema...nina hakika kwamba Mungu ni mwenye haki na kwamba bado ananipenda. Mambo yote hufanya kazi pamoja katika kuwapatia mema wale wampendao Bwana na walioitwa kwa makusudi yake," Alisema Ruth.