Naeza anza kuwa na matatizo ya afya ya akili-Ujumbe wa Shakilla uliowaacha wanamitandao na hisia tofauti

Muhtasari
  • Shakilla pia alifichua kuwa hilo lilimuathiri vibaya kiasi kwamba hivi karibuni anaweza kuanza kuwa na matatizo ya afya ya akili

Sosholaiti mwenye utata Shakilla  ameibua hisia mtandaoni, baada ya kuandika ujumbe wa kutatanisha kuhusu familia yake mwenyewe.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msichana huyo mwenye umri wa miaka 20 alidai kuwa familia yake ilikuwa na sumu na hata kufikia kiwango cha kutamani asingekuwa nao.

Ilipofikia kile kilichochochea kauli yake, sosholaiti huyo  pia alifichua kuwa hakufurahishwa na jinsi jamaa zake hivi majuzi walidaiwa kuelekeza hasira zao kwake.

Shakilla pia alifichua kuwa hilo lilimuathiri vibaya kiasi kwamba hivi karibuni anaweza kuanza kuwa na matatizo ya afya ya akili.

"Naweza kuanza kuwa na matatizo ya afya ya akili , mapema kwa maana hasira za wengine zinaelekezwa kwangu

Familia yenye sumu natamani singekuwa hapa," Aliandika Shakilla.

Hii si mara ya kwanza kwa sosholaiti huyo kulalamika kwa kutokuwa na uhusiano mzuri na wanafamilia yake.

Mapema Februari 2021, akiwa kwenye mahojiano na radiojambo pia alifichua kwa mashabiki wake kwamba hana uhusiano na baba yake mzazi, na kwamba anapendelea ikiwa hatazungumza naye.

Shakila alifichua kwamba akiwa shule ya upili kuna wakati alifukuzwa kwa sababu alikuwa katika kikundi cha wasichana wasagaji.

"Saa hizi nina miaka 18, nakumbuka kuna wakati wazazi wangu walitwa shule baada ya mimi kupatikana nikiwa kwenye kikundi cha wasichana ambao ni wasagaji

 nilijiunga na kikundi hicho kwa ajili rafiki yangu, tulikuwa tunakutana saa tano au nane za usiku kuzungumza maendeleo ya kikundi."