Amber Ray afichua mambo matatu anayoyafanyia kazi hivi sasa Maishani mwake

Muhtasari
  • Amber Ray afichua mambo matatu anayoyafanyia kazi hivi sasa Maishani mwake
Amber Ray
Image: Hisani

Mwanasosholaiti mwenye utata Faith Makau almaarufu Amber Ray amesema kuwa anajiangazia yeye mwenyewe licha ya mazungumzo tanayoedelea mitandaoni ya kuwa amerudiana  na Jimal.

Kulingana naye, kwa sasa anaangazia mambo matatu, moja wapo ni furaha yake.

Pia anaangazia kuhakikisha anajipa matibabu bora yanayostahili. Jambo lingine muhimu ambalo Amber Ray anafanyia kazi ni jinsi ya kutengeneza pesa.

"Ninashughulikia mambo 3 sasa, ubinafsi wangu, furaha yangu na pesa zangu," Aliandika Amberay.

Mara kadhaa, ameripoti kwamba furaha yake inaletwa na pesa; kwa hivyo haishangazi kuona pesa kwenye orodha yake.

Inakumbukwa hata amekataza kuwa hatawahi kuchumbiana na mwanaume ambaye hana pesa.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki baada ya ujumbe wake Amberay'

julie_njoki: Mlisema picha haiko straight ni kiongos Jamal amepiga๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ muda mdogo maneno mengi๐Ÿ•บ๐Ÿ•บ

wanjiru_nw: Your happiness means Jamal๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

nally.j.nallyy: Me napenda relationship yenu nyinyi Co wives. Akiwa kwako yule anaenda vacation.. akirudi kwake wewe unaenda vacation. True meaning of kusaidiana

riziki336: Me nataka aende dubai vacation kama kina mobeto na huddah ndo ntaamini life is for the living