Huwa siwasengenyi wanawake wenzangu-Huddah Monroe

Muhtasari
  • Pia ameweka wazi kwamba huwa hawasengenyi wanawake wenzake, labla mwanamke huyo akiwa amenunua ndege
HUddah Monroe
Image: maktaba

Mwanasosholaiti Huddah Monroe ni miongoni mwa wanawake mashuhuri ambao wanafahamika sana nchini na ata nje za nchi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Huddah amewashauri wanawake kuwafahamu wapenzi wao vyema kabla ya kupata ujauzito wao.

Pia ameweka wazi kwamba huwa hawasengenyi wanawake wenzake, labla mwanamke huyo akiwa amenunua ndege.

"Kama unanijua,unajua huwa siongelelei mwanamke mwenzangu, ata huwa sikubali mazungumzo hayo yaendelee labda mafanikio yao, kuanguka sio sio jambo la kuzungumzia, hatukubalishi nguvu kama hizo," Huddah Alisema.

Huddah amesema kwamba mambo ambayo huzungumza na marafiki zake wa kike ni biashara na jinsi ya kutengeneza ngozi zao.

Aidha amesema hajaona mwanamke ambaye anaweza fanya amsengenye.

"Mazungumzo yangu na wasichana wangu kwa muda mrefu ni kuhusu biashara,vipodozi, jinsi ya ulinda ngozi zao, lakini sio kuhusu mwanamke mwingine

Sijawahi muona mwanamke ambaye anafanya nimsengenye, labda mafanikio yake au amenunua ndege."