'Itachukua muda kuamini sitakuona tena,'Mkewe msanii Guardian Angel amuomboleza dada yake

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Anaeleza jinsi matukio yalivyotokea
  • Namba ya dada yake ilimpigia simu jana asubuhi na alifurahi sana kuwa amepata nafuu lakini haikuwa hivyo
Image: INSTAGRAM// GUARDIAN ANGEL

MKwe msanii wanimbo za ijili Guardian Angel,Esther  Musila alimpoteza dadake jana, tukio chungu ambalo limemwacha akiwa na kiwewe.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Anaeleza jinsi matukio yalivyotokea.

Namba ya dada yake ilimpigia simu jana asubuhi na alifurahi sana kuwa amepata nafuu lakini haikuwa hivyo.

Simu ilipigwa kumjulisha juu ya kifo cha ghafla cha dada yake kipenzi.

Esther anaomboleza ukweli kwamba hatamuona tena dada yake. Anamtaja kuwa mkarimu na mwenye kutoa,Hajui jinsi ya kuishi na ukweli kwamba hayupo tena.

Moyo wake ni mzito na anajuta kwamba hakuwahi kupata nafasi ya kuaga bali anatumai kuwa amepumzika mahali pazuri zaidi.

"Leo ilikuwa nzito 😪 😞. Arciah, sikupata nafasi ya kusema kwakheri na nilipopigiwa simu na namba yako asubuhi ya leo, nilisisimka nikidhani unapiga simu kusema unajisikia nafuu leo, kumbe haikuwa hivyo!!

Sitawahi kukushukuru vya kutosha kwa nyakati ulizopitia kwa ajili yangu. Wewe ndiye dada ambaye sikuwahi kuwa naye

Una moyo mpole zaidi ambao nimewahi kujua. Itachukua muda kuzama ndani sitakuona tena, na ninapopanda ngazi, nyayo zangu zitakua nzito nikipita nje ya mlango wako😢. Ulale salama dada yangu mkubwa. nakupenda."