Ukipata mwanamke ambaye hachepuki dunia hii mshikilie-Amira awashauri wanaume

Muhtasari
  • Katika wadhifa huo pia alijivunia kuwa miongoni mwa wachache, na kudai kuwa kuna wanawake 8 tu wa aina hiyo katika bara zima la Afrika
Image: Studio

Aliyekuwa mke wa Jamal Marlow Amira kupitia akaunti yake ya Instagram amewashauri wanaume wasiwaache wanawake wao waaminifu kwa sababu ni nadra sana kuwapata.

Katika wadhifa huo pia alijivunia kuwa miongoni mwa wachache, na kudai kuwa kuna wanawake 8 tu wa aina hiyo katika bara zima la Afrika.

"Ukipata mwanamke ambae hachepuki dunia hii mshikilie. Tuko nane tu Afrika. Mimi na wenzangu" alisema.

Chapisho la Amira linakuja wiki chache tu baada ya talaka na mumewe wa miaka 17 Jamal Marlow, huku sababu kuu ya kutengana kwao ikiwa kutokuwa mwaminifu katika ndoa yao.

Wawili hao waligonga vichwa vya habari baada ya JImal kumuoa mwanasosholaiti Mber Ray mapema mwaka huu na kisha wakaachana.