Namtafuta!Vera Sidika amsaka mwanamke aliyejaribu 'kumsugua' mumewe

Muhtasari
  • Haya yanajiri baada ya video ya Brown Mauzo na mwanadada fulani kunaswa na kamera wakicheza kwa ukaribu sana
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Vera Sidika amewaonya wanawake dhidi ya 'kumrombosea' au kucheza na mume wake 'handsome'  Brown Mauzo wakati yeye akitumbuiza katika shoo.

Haya yanajiri baada ya video ya Brown Mauzo na mwanadada fulani kunaswa na kamera wakicheza kwa karibu na madaha.

Vera alijibu hasi kwa video hiyo kwa kumwonya msichana mdogo ambaye alikuwa akijaribu kumchezea mumewe.

Vera alimpongeza  mumewe Brown Mauzo kwa onyesho lakini aliwaonya wanawake dhidi ya kuchezea mume wake wakati anatumbuiza katika hafla yoyote.

"Shoo ya mume wangu ilikuwa ya kipekee, lakini namtafuta huyu mwanamke ambaye anajaribu kumrombosea na kusugua mume wangu ambapo anamkimbia na niko hapa na nyonyesha

Nikikushika eeeh, heri ukimbie," Aliandika Vera.