Mimi ni mwanamuziki wacha kufurafura ukiniona na wanaume- Nyota Ndogo amwambia mumewe

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemuonya mumewe Henning Nielsen awache kufura anapomuona na wanaume
nyota ndogo
nyota ndogo

Msanii kutoka mkoa wa pwani Nyota Ndogo, ni miongoni mwa wasanii ambao wamesalia katika tasnia ya usanii kwa miaka mingi sasa.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemuonya mumewe Henning Nielsen awache kufura anapomuona na wanaume.

Nyota amemshauri mumewe kwamba anapaswa kubali kuwa yeye ni mwanamuziki na lazima akue na wasanii wenzake ili wabadilishane mawazo.

Je wanamuziki wanapaswa kukaa na wasanii wenzao ili kubadilisha mawazo na kutoa vibao vikali.

Aidha msanii huyo amemwambia mume wake kwamba anampeza.

Huu hapa ujumbe wake Nyota Ndogo.

"Wewe mbaba nakuomba ujue mimi ni Mwanamuziki. Hivi unaingia kesho na utanikuta nipo bize na tumenyanganyikana na waume"mambo ya kufurafura ukiona wanaume uwache umesikia? Hivi nimekumiss lakini ujue mkeo yupo kazi na sio nyota ndogo jikoni but nyota ndogo wa muziki," Ameandika Nyota Ndogo.