'Mungu hawasahau watu wake,'Nana Owiti asimulia maisha yake ya utotoni

Muhtasari
  • Nana ni msukumo mkubwa sana kwa wasichana wengi wachanga na hata watu wazima haswa wale walio kwenye ndoa changa

Nana Owiti ni mtangazaji wa televisheni, mtu mashuhuri, mama na mke. Ni mke wa King Kaka kwa miaka kadhaa sasa.

Nana ni msukumo mkubwa sana kwa wasichana wengi wachanga na hata watu wazima haswa wale walio kwenye ndoa changa.

Amejithibitishia yeye mwenyewe, mume wake na familia kwamba yeye ni mwanamke mwenye nguvu na anaweza kustahimili aina yoyote ya dhoruba.

Hii ni baada ya kukaa na King bila kuacha kazi alipokuwa mgonjwa sana. Nana alifanikiwa kumtunza hospitalini, kwenda kazini, kuwapeleka watoto wao shuleni na kupanga nyumba yake.

Utafikiri ni malezi magumu aliyopata Nana hadi aendelee kuwa na nguvu. Alilelewa Ukambani ambako anasimulia maisha yalikuwa magumu.

Katika chapisho lake kwenye Instagram, anasimulia jinsi alivyokuwa akienda shule bila viatu na kutembea kwenye mchanga wa moto ambao walilazimika kupaka kinyesi cha ng'ombe kwenye miguu yao ili kulinda nyayo zao.

Bado haamini kwamba alifanikiwa na kuishi maisha mazuri sana. Anamshukuru Mungu na kwa hakika anampa Yeye utukufu wote.

"Ata siaminingi nikiwa mtoto, nilitembea shuleni bila viatu. Ardhi ingekuwa na joto kali (Laumu hali ya hewa ya UK-UKAMBANI 😆 ) hivi kwamba kungekuwa na mvuke unaotengenezwa kutoka kwenye udongo

Tungekimbia, tujifiche chini ya miti(ambayo ilikuwa inahesabika.Wakamba tupande kitu tafadhali sijui jinsi sikuweza kuwa 'Kipchoge wa kike)

Hata hivyo, jambo jema, Mungu hawasahau watu wake. Siwezi kuhesabu idadi tuliyomwimbia Mungu nje ya kahome yetu kwa Thome(men’s place of chilling)Mwezi ulikuwa unang’aa na pia sauti zetu. Yaani.. niseme tu, Haijalishi tunatoka wapi, Mungu ndiye mwanzilishi wa maisha yetu ✍️," Alisema Nana.