Gereza mbaya zaidi ulimwenguni ni nyumba isiyo na amani-Amira asema

Muhtasari
  • Kweli ikiwa wewe ni mfuasi wake kwenye akaunti yake ya Instagram, basi lazima utakuwa umeona jinsi ambavyo amekuwa akifurahia
Amira
Image: Hisani

Siyo siri kwamba mshawishi wa chapa Amira sasa anaishi maisha ya furaha tangu alipotalikiana na mume wake ambaye pia ni mfanyabiashara Jamal Marlow.

Kweli ikiwa wewe ni mfuasi wake kwenye akaunti yake ya Instagram, basi lazima utakuwa umeona jinsi ambavyo amekuwa akifurahia kwa kwenda likizo Uganda, Tanzania na Zanzibar.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amesimulia kwa njia isiyo ya moja kwa moja jinsi maisha yake ya ndoa na mwenyekiti wa Chama cha Waendeshaji Matatu yalivyokuwa, na akayafananisha na gereza mbaya zaidi ulimwenguni kwa sababu lilikuwa na hakuna amani.

"Gereza mbaya zaidi duniani ni nyumba isiyo na amani" aliandika.

Kwa sehemu kubwa ya mwaka huu ndoa ya Amira ya miaka 17 na Jamal Marlow ilikuwa na msukosuko mkubwa, na hii yote ni kwa sababu aliamua kuoa mwanasosholaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray kama mke wake wa pili.