'Huwa natumiwa video za vitisho,'Nyota Ndogo ajibu madai ya kumtupa mama yake

Muhtasari
  • Nyota Ndogo ajibu madai ya kumtupa mama yake

Mwimbaji wa Mombasa Nyota Ndogo alimjengea mamake nyumba miaka michache iliyopita na hata kushiriki picha nzuri za nyumba hiyo.

Kulingana na chapisho la kwenye ukurasa wake wa instagram inaonekana kana kwamba kuna mtu ambaye anajaribu kumtishia kwa kupakia video.

Amesema kuwa baadhi ya watu wamesema watachapisha kuhusu yeye kutomjali mama yake mzazi, na hii si kweli kwa mujibu wake.

Anajenga nyumba ya mama yake na hutoa kila mara. elfu kumi yake kila mwezi kwa ajili ya malezi yake, hii inapaswa kuwa zaidi ya kutosha kwa sababu baada ya yote yeye si mtoto pekee.

Alisema moyo wake uko safi ukizingatia suala hilo na anayetaka kumuweka wazi afanye hivyo, kwa kuwa muziki wake haufanyi vizuri anatumia pesa zake za biashara ya hoteli kumtunza mama yake.

"NIMEMJENGEA MAMANGU NYUMBA KISHA KILA MWEZI NAMPA ELFU KUMI YA MATUMIZI.MUNATAKA NIFANYE NINI ZAIDI YA HAYA JAMANI.

Nimeshangazwa kuamka asubuhi kukuta watu wanasema vile nimemtupa mamangu. Kweli mimi navyopenda kusaidia jamii naweza shindwa kuangalia mamangu?

Mtu anasema kabisa yupo tayari kufungwa anahuhakika kuwa simuangalii mama? Mimi mpaka natumiwaga video za vitisho za kuambiwa tutapost tukuaibishe lakini nanyamaza tu cause ninajijua

Munaweza hata kupeleka waandishi wa habari kwa mamangu anapoishi atawaeleza mwenyewe. NIMEMJENGEA MAMA NYUMBA, HII HAPA, NA KILA MWEZI NAMPA 10K ya matumizi

Sina pesa za muziki ila pesa natoa katika biashara yangu ya hoteli. Nyie mnao jipiga kifua jifunzeni kutafuta ukweli

Alafu mama hakunizaa pekeangu, tupo wanawake wanne na wavulana wawili. Mbona mniandame mimi tu? Kweli, KUWA STAR NI MZIGO SANA!!!"Alisema Nyota.