Mliambiwa hata mawe kuna siku zitaimba,'Diana awatania mashabiki huku akidai amehamasisha wengi tangu aanze kuimba

Muhtasari
  • Diana Marua adai amehamasisha wengi tangu ajitose kwenye muziki
Diana Marua
Image: Hisani

Diana Marua maarufu Diana B amekuwa akivuma kwa muda sasa baada ya kujitosa kwenye tasnia ya muziki.

Kujitosa kwake hakukupokelewa vyema na mashabiki, kwani alipokea kejeli nyingi kuliko sifa,Diana hakujali kile wanamitandao wanasma bali aliendelea na kutoa vibao moja baada ya kingine na kupokelewa vyema na mashabiki.

Wiki iliyopita Diana alizidi na kuvuma baada ya kudai kwamba msanii mwenzake Willy Paul alijaribu kunyanyasa kingono.

Leo kwenye ukurasa wake wa instagram amewatania mashabiki huku akiwaambia kwamba waliambiwa kuna siku mawe yatainuka na kuimba wakadhani ni mchezo.

Pia alidai kwamba amehamasisha watu wengi tangu aanze kuimba, kupitia kwenye video yake nyingine alisema kwamba anajitahidi kwe ye kazi yake ya usanii ili kuwahakikishia wanawake kwamba kila kitu kinawezekana.

"Tangu Nianze Kuimba, nimehamasisha Kila Mtu na Kila Kitu... Hata Wanyama kuanza kuimba 😂😂😂😂😂😂

Mmmmmhhh, si mliambiwa "hata mawe kuna siku zitaimba" mkabishana... Ona maisha yako oooohhh 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Nilipata jeshi nyuma yangu. Jana usiku Show yangu pale Avery Lounge ilikuwa moto siku chache tu kwenye tasnia ya muziki na upendo ninaopokea kutoka kwa mashabiki na wafuatiliaji kote nchini ni balaa😍

Nitaendelea kusukuma kwa bidii kuwaonyesha wanawake wote kwamba hakuna lisilowezekana," Aliandika Diana.