Utakuwa moyoni mwangu milele,'Amberay asema huku akimuomboleza rafikiye

Muhtasari
  • Mwanasosholaitii Amber Ray anajulikana kuwa malkia mwenye furaha ambaye huwa haruhusu muda wowote kupita bila kuufanya kuwa wa maana
  • Hata alijiita balozi wa maisha laini na kila mara hutumia msemo 'life is or the living'
Amber Ray
Image: Hisani

Mwanasosholaitii Amber Ray anajulikana kuwa malkia mwenye furaha ambaye huwa haruhusu muda wowote kupita bila kuufanya kuwa wa maana.

Hata alijiita balozi wa maisha laini na kila mara hutumia msemo 'life is or the living.'

Hata hivyo,  Kupitia ukurasa wake wa Instagram, malkia huyu mkali alishiriki video alizochukua na rafiki yake wa karibu  ambaye sasa ni marehemu anayeitwa Sally.

Kutoka kwa chapisho hilo la kuhuzunisha, Amber alilia kwa sababu kifo cha Sally kilikuwa kimetarajiwa na kiliacha shimo kubwa moyoni mwake.

Maelezo yake yalisomeka:

"Nilikuwa na rafiki, dada, mshangiliaji, mshirika katika uhalifu, nguzo, mshauri, mshirika wa maombi, na hata ulinifanya niamini kuwa mtu mzuri bado yupo. Nitafanya nini na shimo hili kubwa uliloniacha nalo. Haitakuwa sawa kamwe

Nimekupeza tayari mpenzi….lakini nitashikilia kumbukumbu nzuri hadi tukutane tena. Nakupenda milele. R.I.P. BFF," Amber Aliandika.