Njugush na mkewe waadhimisha miaka mitano katika ndoa

Muhtasari

•Wanandoa hao waliadhimisha miaka mitano katika ndoa siku ya Alhamisi.

Image: INSTAGRAM// CELESTINE NDINDA

Mwigizaji na mchekeshaji mashuhuri Timothy Kimani almaarufu kama Njugush pamoja na mke wake Celestine Ndinda walisherehekea maadhimisho ya ndoa yao.

Wanandoa hao waliadhimisha miaka mitano katika ndoa siku ya Alhamisi.

Ndinda alijitosa mitandaoni kumsherehekea mumewe pamoja na ndoa yao kwa ujumbe maalum. Mama huyo wa mtoto mmoja alisema anafurahia sana kuwa na Njugush maishani.

"Kheri za kumbukumbu ya miaka 5 ya ndoa yetu @blessednjugush. Nimebarikiwa sana kufanya kitu hiki kinachoitwa maisha na wewe. Cheers to more!!!" Ndinda aliandika.

Njugush pia alisherehekea siku hiyo ya furaha kwao kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Wanandoa hao walifunga pingu za maisha mwaka wa 2016 na tayari wamebarikiwa na mtoto mmoja anayejulikana kama Tugi.

Mamia ya wanamitandao ikiwemo watu mashuhuri wameendelea kuwasherehekea wawili hao kwa jumbe nzuri na kuwatakia maisha marefu ya ndoa.

@carrolradull Aww Hongera! Kheri za maadhimisho ya ndoa kwenu wawili @celestinendinda

@davidtmuguro Kheri za maadhimisho ya ndoa mashujaa wa mapinduzi.

@ladybee_254 Wooo Kheri za maadhimisho ya ndoa, baraka tele kwenu

@jahmbykoikai Kheri za maadhimisho ya ndoa kwenu wawili familia. Upendo mkubwa na Mungu awabariki sana.