"Kwa rafiki yangu mkubwa.." Itumbi amwandikia Jacque Maribe shairi tamu anapoadhimisha siku ya kuzaliwa

Muhtasari

•Msemaji huyo wa 'Hustler Nation' amemtaja Maribe kama mwanamke jasiri huku akimtakia mafanikio makubwa, furaha tele na upendo.

•Mara nyingi Itumbi ameonyesha upendo mkubwa alio nao kwa mtangazaji huyo  huku akionekana kusimama naye hata katika nyakati ngumu

Dennis Itumbi, Jacque Maribe na Jowie Irungu
Dennis Itumbi, Jacque Maribe na Jowie Irungu
Image: MAKTABA

Mtangazaji Jacque Maribe anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa leo (Jumamosi, Desemba 18).

Marafiki pamoja na wanamitandao wameendelea kumtumia mama huyo wa mtoto mmoja jumbe za kumtakia kheri za siku ya kuzaliwa na kumuombea maisha marefu.

Rafiki wake wa karibu na ambaye inaaminika amewahi kuwa naye kwenye mahusiano Dennis Itumbi hajaachwa nyuma huku akimnakilia shairi ya kupendeza katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Itumbi amemsifia sana Maribe kutokana na ujasiri ambao ameonyesha katika kupambana na magumu ambayo yamemkabili kipindi cha miaka mitatu ambacho kimepita.

Msemaji huyo wa 'Hustler Nation' amemtaja Maribe kama mwanamke jasiri huku akimtakia mafanikio makubwa, furaha tele na upendo.

"Kwa rafiki yangu mkubwa, Jacque Maribe, Heri ya Siku ya Kuzaliwa.

Kwa miaka mingi, haswa kutoka 2018, umejitokeza kama mpiganaji!

Msichana, tulipojaribu kuwa kivuli, tuligundua wewe ni jua,

Umekuwa MOTO siku zote,

Labda miale ya moto zaidi,

Lakini kwa mwaka huu,

Nguvu zako haziwezi kustahimili,

Unastahili kila aina ya vivuli,

Hata kama wewe ni Jua,

Nakutakia mapigano machache,

Ushindi zaidi na kicheko,

Mapambano machache,

Ushindi zaidi,

Furaha na kukumbatiwa kabisa,

Mapenzi na Orgasms pia..

HERI YA KUZALIWA! " Itumbi aliandika.

Mara nyingi Itumbi ameonyesha upendo mkubwa alio nao kwa mtangazaji huyo  huku akionekana kusimama naye hata katika nyakati ngumu, k.m wakati alipokuwa ametiwa mbaroni baada ya kuhusishwa na mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani.