Tunapambana sana-Nadia Mukami ajibu madai ya kutolewa jukwaani akitumbuiza mashabiki Mombasa

Muhtasari
  • Nadia Mukami ajibu madai ya kutolewa jukwaani akitumbuiza mashabiki Mombasa
Nadia MUkami
Image: Hisani

Nadia Mukami ni mmoja wa wanamuziki bora zaidi wa kike tulio nao hapa Kenya. Mengi yamekuwa yakifanywa mitandaoni na waliohudhuria onyesho lao la Jumamosi usiku mjini Mombasa.

Ambapo walikuwa wakitumbuiza pamoja na Masauti na Mbosso  na wasanii wengine.

Shabiki mmoja alidai kuwa alipokuwa akitumbuiza, alitolewa nje ya jukwaa kwa lengo la kumtengenezea njia Mbosso.

Ambaye pia alipangwa kutumbuiza na lilikuwa kosa lake tangu aje akiwa amechelewa. Walitolewa nje ya jukwaa baada ya kutumbuiza kwa muda mfupi tu.

"Hawa wasanii wa kenya  wataendelea tu kuumia na Kudharauliwa mpaka SIKU ile wataniskia...Asiye skia la Mkuu Huvunjika guu...Anyway Plans are underway to BRING UP a TOTALLY NEW BREED of MUSICIANS hawa WASHATUANGUSHA," Alisema Eric baada ya kupata habari za tukio hilo.

Ameamua kuzungumzia suala hilo, baada ya Eric Omondi kuamua kuingilia kati. Ambaye aliona kama waliteswa kwa ajili ya msanii wa kigeni.

Akisema kuwa hahitaji kugombana na mapromota ili kuonyesha kuwa anapigania haki yake ya msanii.

Pia Nadia alisema kwamba kuna baadhi ya mambo ambayo hayahitaji vita

"@ericomondi ulikuwa unataka mimi na Masauti tupige promoter ndio mjue we are fighting for the industry ama??? Kuna vitu havitaji kifua!! Tunapambana sana!! Una hoja halali ya kupush mapigano kulinda tasnia yetu lakini jinsi unavyoikaribia wakati mwingine ni meeeeh tu!!! Acha kufanya pambano la Eric Omondi!! Ni mazungumzo ya tasnia !!! Hiyo inahitaji mifumo mingi na ujenzi wa muundo," Alijibu Nadia.