Unapopata watu wawili wakiwa wamefurahi pamoja tafadhali waache-Anerlisa Muigai asisitiza

Muhtasari
  • Mrithi wa Kampuni ya Keroche Breweries Anerlisa Muigai amewataka wakosoaji kukaa mbali na uhusiano wa watu

Mrithi wa Kampuni ya Keroche Breweries Anerlisa Muigai amewataka wakosoaji kukaa mbali na uhusiano wa watu.

Kulingana naye, ni dhabihu kubwa kufanya mambo yaende katika uhusiano, kwa hivyo wawili hao wanapofurahi, wanapaswa kuachwa peke yao.

"Unapopata watu wawili wakiwa wamefurahi pamoja tafadhali waache...watu hawajui ni bidii ngapi inafanywa ili kufanya mambo yaende," Alisema Anerlisa.

 Katika chapisho tofauti, aliorodhesha mapenzi yanajumuisha nini. Katika orodha hiyo, alitoa heshima, urafiki, na uelewano. Pia alijumuisha mawasiliano na ushirika kama sehemu kuu za upendo.

"Upendo ni mchanganyiko wa heshima, urafiki, maelewano, mawasiliano na ushirika."

Mfanyibiashara huyo alifahamika sana baada ya kumpoteza dada yake, na baada ya kutalikiana na mumewe.

Hivi majuzi akiwahutubia wanahabari Tanzania Anerlisa alidai kwamba ndoa ni jambo la kupewa heshima na wala sio la kuongelelea kila mara na kila mtu.