Aliniacha na mtoto mchanga baada ya kumchukulia mkopo wa Sh 500,000-Mwanamume asimulia

Muhtasari
  • Mwanamitandao mmoja alisimulia jinsi aliachwa na mkewe baada ya kumchuklia mkopo wa kuanzisha biashara
sad man
sad man

'Mtaachana tu,' ni kauli ambayo inatumiwa sana na imekuwa ikitumiwa mitaani na wapendanao, hasa kwa wale walioachana, huku wakiwakejeli wenye wako kwa uhusiano wa kimapenzi.

Kupitia wenye mitandao ya kijamii, wanamitandao walisimulia sababu yao kuu ya kuachwa na waliokuwa wapenzi wao.

Mwanamitandao mmoja alisimulia jinsi aliachwa na mkewe baada ya kumchuklia mkopo wa kuanzisha biashara.

Huu hapa usimulizi wake;

"Ni siku ambayo iko kwenye nyayo za akili yangu, kwani nilimchukulia mke wangu mkopo wa shilingi elfu mia tano ili aweze kuanzisha biashara yake ambayo tulikuwa tunazungumzia kwa muda

 Baada ya kupata pesa hizo aliniacha na mtoto wa mwaka mmoja na kuzima simu kwa miezi kadhaa, sikufahamu kwamba huo ndio ulikuwa mpango wake, kilichonihumiza roho ni kuwa alitoroka na mwanamume mwingine wakaenda kuanzisha maisha yao," Alieleza Mwanamume huyo.

Mwanamitandao mwingine anaye alisimulia na kusema kuwa;

"Iliniuma sana kwa sababu aliniacha nilipokuwa namhitaji sana yaani nilikuwa mgonjwa singeweza kujisaidia, alirudi nyumbani na kuniambia hawezi ishi na mwanamke ambaye ni kama kiwete kwake

Lakini masha yashaasonga," Alieleza.

Haya basi wadau chungeni na mkae macho ni wakati wa sikukuu, na unaweza wachwa kwa sababu ndogo sana.

Je kwa nini mpenzi wako wa awali alikuacha?