Kumpenda mtu aliyeamua kuacha bibi yake sio kukosa heshima-Fridah Kajala awaonya wanaomkejeli mwanawe

Muhtasari
  • Hii ni baada ya madai kwamba alivunja ndoa  kati ya msanii Rayvanny na baby mama wake Fahyvanny
Paula Kajala na FRida Kajala
Image: Frida Kajala/INSTAGRAM

Fridah Kajala anajulikana kwa kushughulikia masuala yake mengi mtandaoni . Na iwe inamhusu yeye au binti yake anazizungumzia  kupitia Instagram live au hadithi za Instagram.

Fridah alifahamika sana kupitia kazi yake ya uigizaji, ilhali aligonga vichwa vya habari baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa bongo Harmonize, na baada ya muda mfupi wakaachana.

Leo asubuhi na mapema sana Fridah Kajala amechukua hatua kuwahutubia wanaomchukia wanaosema kuwa bintiye hana heshima kwa wazee .

Hii ni baada ya madai kwamba alivunja ndoa  kati ya msanii Rayvanny na baby mama wake Fahyvanny.

Fridah kwa hisia aliwaomba watu waache kumtuhumu binti yake kwani alisema mapenzi hayana mipaka.

Rayvanny na baby mama wake waliachana mapema mwaka huu, huku akiaznisha uhusiano wa kimapenzi na mwanawe Fridah Kajala, Paula Kajala.

Uhusiano wao haukupokelwa vyema na wanamitandao kwani walimshambulia Paula.

"Nimemlea Vizuri Sana na ana heshima zake kwa wazee na kila mtu . Kumpenda mtu aliyeamua kuacha bibi yake sio kukosa heshima mapenzi hayana mipaka," Fridah Alisema.