Najua watoto wako salama,ninaahidi nitakuwepo kwa ajili yao watakaponihitaji -Amber Ray asema huku akimuomboleza rafikiye

Muhtasari
  • Kwa mujibu wake Amberay atawasaidia wanawe kila wakati, huku akikiri kwamba kifo cha Sally kimemfunza mambo muhimu maishani
Amber Ray
Image: Hisani

Mwanasosholaiti Amberay kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, alizidi kumuomboleza rafiki yakke Sally.

Sally alizikwa siku ya JUmanne.

Kwa mujibu wake Amberay atawasaidia wanawe kila wakati, huku akikiri kwamba kifo cha Sally kimemfunza mambo muhimu maishani.

"Tunapopoteza mpendwa, kipande chetu hufa pamoja naye, lakini bado wanaishi ndani yetu. Kukubali kupoteza hakuna hasara yenyewe. Kukubali hasara ni kuona kwamba uchungu unaohisi ni upendo mwingi unaouhisi kwa Sally sasa kwa kuwa yuko karibu nasi zaidi kuliko hapo awali. Sasa yuko kwa njia ambazo hazijazoeleka na hazielezeki hata kwetu. Na kumbukumbu zetu za zamani zitupe nafasi ya kumuona Sally jinsi alivyo sasa hivi.

Mpendwa wangu Sally, ulikuwa na mimi kila wakati! Uliniangalia kila wakati! Sasa ni zamu yangu kukufanya ujivunie hapa duniani.

Najua watoto wako salama na kaka yako John na Dada Imani! Pamoja na familia yako yote."

Aliedela na ujumbe wake;

"Najua viwango ambavyo tayari umewawekea vitakua tu, na ninaahidi nitakuwepo kwa ajili yao watakaponihitaji na hata wasiponihitaji.

Yesu alienda kutuandalia mahali, nadhani yako iliisha kabla yangu kwa sababu fulani, kwa hivyo tafadhali waonyeshe jinsi ninavyopenda mambo yangu ya ndani kufanywa, na mahali pa kuweka jikoni.

Huzuni tunayoipata leo ni zaidi ya kifo chako kikitukumbusha kuwa tunaelekea huko.

Kifo chako kimenifundisha mambo muhimu, Kimenifundisha ni nani wa maana, na kimenikumbusha kwa nini ni muhimu.

Nenda vizuri rafiki yangu, na safari yako mpya iwe ya kupendeza kama wewe," Aliandika Amberay.