Kutana na wacheshi na waigizaji waliojitosa kwenye tasnia ya muziki 2021

Muhtasari
  • Tasnia ya muziki mwaka wa 2021 imekuwa na changamoto nyingi, huku baadhi ya wasanii wakitafuta kiki kwa ajili ya vibao vyao
mammito
mammito

Tasnia ya muziki mwaka wa 2021 imekuwa na changamoto nyingi, huku baadhi ya wasanii wakitafuta kiki kwa ajili ya vibao vyao.

Bali na kiki tumewaona wengi wakitia bidii katika kazi zao na kutoa kibao kimoja baada ya kingine.

Pia tumewaona waigizaji, waheshi nchini wakijitosa kwenye tasnia ya muziki, sijui ni kwa ajili yao kutaka kuwa wasanii ama wanataka kujifurahisha, lakini wakati utuambia.

1.Mammito

Mammito ni mcheshi wa kike kutoka Kenya ambaye amekuwa akitamba katika ulingo wa vichekesho kwa muda. 

Siku ya Jumanne Mammito alitoa kibao ambacho kinafanya vyema kwenye mitandao ya Youtube, na kuahidi kwamba yuko tayari kutoa kibao kingine.

2.Diana Marua

Kwa sasa anajiita Diana B,kujitosa kwake kwenye tasnia ya muziki hakukupoke;ewa vyema na mashabiki bali alizidi kukaza kamba na kutoa vibao 2.

3.Professor Hamo

Profesa Hamo mapema mwaka huu alikuwa na kashfa ya DNA na mkewe Jemutai.Huku akiacha kazi yake ya utangazaji.

Hamo alitoa kibao chake cha kwanza wiki jana.

4.Catherine Kamau

Ametoa wimbo unaoitwa Ndoa hapo awali pamoja na Mr.Seed.Bado hajatoa nyingine lakini pia ni mmoja wa waigizaji waliojiunga na muziki siku za hivi karibuni. 

Je kwa maoni yako hawa watawezana na tasnia ya muziki na chngamoto na kuwapa mashabiki matarajio yao?