Baadhi ya wasanii mashuhuri nchini ambao wamewahi kuchumbia/kufunga ndoa na wapenzi wazungu

Muhtasari

•Mwanamuziki Esther Akoth almaarufu kama Akothee amewahi kuwa kwenye mahusiano na wanaume wawili wenye asili ya Ulaya na hata kupata watoto nao.

Willy Paul, Akothee, Nyota Ndogo, Lenana Kariba
Willy Paul, Akothee, Nyota Ndogo, Lenana Kariba
Image: INSTAGRAM

Willy Paul

Mwanamuziki Wilson Radido almaaarufu kama Willy Paul amewahi kuwa kwenye mahusiano na mwanadada kutoka Urusi anayetambulika kama Victoria Shcheglova.

Katika mahojiano ambayo amekuwa akifanya  imeonekana kama kwamba mwanamuziki huyo bado anamchumbia Mrusi huyo. 

Willy Paul alimshirikisha Victoria katika video ya wimbo wake wa hivi majuzi 'My Woman'

Wawili hao hata wamebarikiwa na binti mmoja. 

Willy Paul alitangaza kuzaliwa kwa binti yao Sonya Wilsovna mwishoni mwa mwaka uliopita.

Hata hivyo, staa huyo mwenye umri wa miaka 28 anajulikana kuweka mahusiano yake siri na hali ya mahusiano yao haifahamiki wazi ilivyo.

Akothee

Mwanamuziki Esther Akoth almaarufu kama Akothee amewahi kuwa kwenye mahusiano na wanaume wawili wenye asili ya Ulaya na hata kupata watoto nao.

Mama huyo amewahi kumchumbia Bw Dominic kutoka ufaransa na mwanamume mwingine kutoka Uswizi.

Prince Ojwang na Prince Oyoo ni watoto ambao msanii huyo alipata kutoka kwa mahusiano yake na wazungu wawili.

Nyota Ndogo

Mwanamuziki Mwanaisha Abdalla almaarufu kama Nyota Ndogo amekuwa akiweka hadharani mahusiano wake na mumewe mzungu kutoka Netherlands.

Nyota Ndogo na Bw Henning Nielsen walijitosa kwenye mahusiano zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Mwaka huu uhusiano kati ya wawili hao umekuwa ukiangaziwa sana kwani kuna wakati ulionekana kuyumba.

Bw Henning yumo nchini Kenya kwa sasa kusherehekea likizo ya Krimasi na mwanamuziki huyo kutoka Pwani.

Lenana Kariba

Mwigizaji mashuhuri Lenana Kariba alifunga pingu za maisha na mpenzi wake Helen mwezi Septemba mwaka huu.

Mwigizaji huyo ambaye kwa sasa anaishi Uingereza alivisha  pete mzaliwa huyo wa Netherlands katika visiwa vya Carribean.

Octopizzo

Image: HISANI

Rapa Henry Ohanga almaarufu kama Octopizzo amefunga ndoa na mwanadada mzungu ambaye wamebarikiwa na watoto watatu pamoja; Zara, Tracy na Fredy.

Anita Nderu

Mtangazaji Anita Nderu alifunga pingu za maisha na mpenzi wake Barrett Raftery  mwezi Septemba mwakani katika hafla iliyohudhuriwa na wanafamilia na marafiki wachache.

Barret ambaye ni mwanamazingira ana asili ya Kihindi.