Lala salama:Meneja wake msanii Rayvanny ampoteza baba yake

Muhtasari
  • Meneja wake msanii Rayvanny ampoteza baba yake
  • Kwa mujibu wa chapisho iliyosambazwa na Wasafi kupitia ukurasa wao wa Instagram, vijana hao walikuwa wakipitisha taarifa hizi za kusikitisha kuhusiana na kifo cha babake Don Fumbwe

Kifo kimetokea tena na kumtia majonzi mazito mmoja wa mameneja wa Wasafi, baada ya kumpoteza baba yake.

Kwa mujibu wa chapisho iliyosambazwa na Wasafi kupitia ukurasa wao wa Instagram, vijana hao walikuwa wakipitisha taarifa hizi za kusikitisha kuhusiana na kifo cha babake Don Fumbwe ambaye alifariki jana alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kumbuka, Don Fumbwe ni mmoja wa mameneja wa Wasafi ambaye anamsimamia Rayvanny.

Sasa habari hii ya kusikitisha kuhusu kifo cha babake Don Fumbwe imeenea kwenye mitandao tofauti ya kijamii ambapo, inazua hisia tofauti kwa sasa.

Wengi wamejitokeza kutuma salamu zao za rambirambi kwa familia na marafiki wa Don Fumbwe katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.

"#TANZIA @donfumbwe ambaye ni Manager Wa Star Wa Muziki Barani Africa @rayvanny, Amefiwa na Baba Yake Mzazi Mzee Jumaa Fumbwe ambaye alifariki Jana jioni katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa Matibabu

Mazishi yatafanyika Kesho Alhamisi Januari 6, 2022 Nyumbani Kwao Makorora Gatundu, Jijini Tanga

Wasafi Media Tunatoa Pole Kwa @donfumbwe Pamoja na Familia, Ndugu, Jamaa Na Marafiki Katika Kipindi Hiki Kigumu

Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amin."