'Nitakupeza sana,'Otile Brown ampoteza nyanya yake

Muhtasari
  • Msanii maarufu Otile Brown kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ametangaza kifo cha nyanya yake

Msanii maarufu Otile Brown kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ametangaza kifo cha nyanya yake.

Otile mwaka jana akiwa akwenye mahojiano alisema kwamba amelelewa, na nyanya yake baada ya wazazi wake kuaga dunia baada akiwe na umri wa chini.

Ni habari ambazo zimewaacha mashabiki wake wakituma risala za rambi rambi kwa msanii huyo.

"Ametuacha asubuhi ya leo nitakupeza malkia, asante," Aliandika Otile.

Otile anafahamika sana mitandaoni kutokana na bidii ya kazi yake, na usanii wake.

Ni miongoni mwa wasanii ambao hawajakuwa wakitafuta kiki ili kuendeleza kazi yao au ili vibao vyao vivume.