Ebu mniache,'Wema Sepetu awaambia wakosoaji wake mitandaoni

Muhtasari
  • KUlingana na mashabiki wengi ujumbe huo ulikuwa unawaendea ambao wamekuwa wakimkosoa na kumkejeli

Tunapomzungumzia Wema Sepetu wengi wanamfahamu kama mpenzi wa zamani wa staa wa bongo Diamond Platnumz.

Baadhi ya wanamitandao wamekuwa wakimkejeli mjasirimali huyo kwa kutokuwa na mtoto maishani mwake licha ya kuwachumbia wanaume maarufu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagrma Sepetu amewakomesha washambuliaji wake na kuwaambia kwamba wanapaswa kumuacha peke yake.

KUlingana na mashabiki wengi ujumbe huo ulikuwa unawaendea ambao wamekuwa wakimkosoa na kumkejeli.

"Yaani Binadam bwana, Usipofanya wanasema, Ukifanya pia wanasema.... Sasa sijui hata nifanye nn🙄🙄🙄... Ebu mniache... Haya basi tufanyeni 7Kichwa Challenge.... Maana nimewachoka for real..." Aliandika Wema Sepetu.

Ni wazi kuwa Sepetu alikuwa mpenzi wake Diamond, mapenzi ya wawili hao yalitamanika na wengi bali hawakukaa waliachana baada ya muda.

Miazi chache iliyopita wema alikiri kwamba yuko 'single' na anapeza kumpenda mtu.