'Mungu abariki roho yako,'Ujumbe wa Diana Marua kwa Milly Chebby anapoadhimisha siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Ujumbe wa Diana Marua kwa Milly Chebby anapoadhimisha siku yake ya kuzaliwa
  • Pia msanii huyo alifichua kwamba kuna mambo mengi ambayo wamepanga kufanya pamoja mwaka huu, na anafuraha sana
Milly Chebby
Image: Milly Chebby/INSTAGRAM

Huku mkewe Terence Creative, Milly Chebby akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa, mashabiki,marafiki wa karibu na hata mashabiki wamemtakia kheri njema siku yake ya kuzaliwa.

Diana Marua kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alimsherehekea Milly, huku akimtakia Mungu aibariki rogo yake.

Kulingana na Marua, alimfahamu Milly kupitia kwenye kipindi chake cha kupika, ambacho kilimshinikiza sana na kumtia moyo.

Pia msanii huyo alifichua kwamba kuna mambo mengi ambayo wamepanga kufanya pamoja mwaka huu, na anafuraha sana.

"Heri ya Siku ya Kuzaliwa kwa mmoja wa watu wazuri na wa kushangaza ambao Mungu ameweka katika ulimwengu huu.

@millychebby alikuwa "rafiki" mtandaoni ambaye alinitia moyo kupitia chaneli yake ya upishi. Nilivutiwa na Risiti zake, ninachopenda ni kuku Biryani 😋

Tulikutana kitambo na nilipenda nguvu na chanya yake kwa kila kitu na mengine, sasa ni mambo makubwa ambayo tumepanga kushiriki na nyinyi mwaka huu, nimefurahi!!!

@millychebby Mungu Abariki moyo wako na lizidi kuwa fungu lako siku zote za maisha yako. HERI YA SIKU YA KUZALIWA MREMBO ♥️," Aliandika Marua.