Nataka dem anaeza zaa watoto saba-Ringtone adai

Muhtasari
  • Mwanamuziki wa Injili Alex Apoko akiwa kwenye mahojano alisema kuwa bado hajaoa na hatafuti lakini akaongeza kuwa anajiona akioa ndani ya miaka mitatu
ringtone apoko
ringtone apoko

Mwanamuziki wa Injili Alex Apoko akiwa kwenye mahojano alisema kuwa bado hajaoa na hatafuti lakini akaongeza kuwa anajiona akioa ndani ya miaka mitatu.

Alipoulizwa kuhusu aina ya mwanamke ambaye angependa kuwa naye, Ringtone Apoko alijibu kwa kusema kwamba anataka mwanamke ambaye anaweza kusali kwa saa saba na awe na uwezo wa kuzaa watoto saba na kuendelea.

Alisema kuwa "Nataka dem anaeza zaa watoto saba na kuendelea."

Apoko alisema zaidi kwamba hayo ndiyo mahitaji ya chini kabisa kwa mke wake mtarajiwa.

Msanii huyo pia alijigamba na kusema kwamba yeye amechaguliwa na Mungu kutangaza neno lake kwa watu wa kenya na zaidi ya yote kuendelea tasnia ya nyimbo za injili.

"Kama akina Bahati,Willy Paul na Mr Seed wanapotosha tasnia ya injili, lakini Mungu anataka Mwanamume mmoja kufanya kazi yake."

Aidha alisema kuwa changamoto yake kubwa sasa ni kumtafuta bibi, kwani wanawake wa sasa hawajui kutumia pesa vyema.