Nilikuwa nadhani mimi ni msanii mkubwa-Jaguar afunguka jinsi alifukuzwa Marekani kama mwanamuziki

Muhtasari
  • Alisema kuwa wakati huu alijaribu kuingia kwenye muziki na akatoa nyimbo kadhaa ambazo hazikufanya vizuri
JaguarJ.000
JaguarJ.000

Mbunge wa Starehe Charles Njagua almaarufu Jaguar amezungumza kuhusu mwanzo wake duni, eneo la maisha yake ambalo ameweka mbali na umma kwa ujumla.

Katika mahojiano na Willy M Tuva, mwanamuziki huyo tajiri alieleza jinsi alivyoanza kwa kufanya kazi za kuosha magari kabla ya kufanya kazi ya maknga.

Alisema kuwa wakati huu alijaribu kuingia kwenye muziki na akatoa nyimbo kadhaa ambazo hazikufanya vizuri.

Mwanamuziki huyo baadaye alisafiri Marekani, akiendelea kujaribu kuendeleza kazi yake ya muziki.

“Kufika Detroit nilikuwa na kiherehere nilikuwa nadhani mimi ni msanii mkubwa sana kwa sababu nilikuwa nimepata invite kutoka kwa rafiki yangu kwa sababu alikuwa anaskia mimi huimba, kufika kule ata sikuwa na ATM card yenye ina visa,” said the Starehe legislator.

Sasa ma-askari wa kule wakaniuliza sema ukose mtu kwenye airport utatumia pesa gani na wakanirudisha mpaka Kenya.”

Hata hivyo, mbunge huyo hakukata tamaa na alirejea ubalozini kupata nyaraka sahihi na kila alichohitaji ili kurejea Marekani kwa ajili ya nyota yake.

"Nilirudi kwa Embassy kwa sababu sikukata tamaa," Alisema Jaguar.

Nchini Marekani, mtumbuizaji huyo wa zamani aligundua kuwa watu hawakumjua na hivyo akaanza kufanya kazi ya mikono ili aendelee kuishi.

Kulingana na Jaguar, alibadili hali hiyo ya kidonda kwa manufaa yake na kusababisha apate milioni yake ya kwanza ambayo kisha alitumia kuanzisha biashara ya teksi nchini Kenya na baadaye kampuni ya gereji.

“Kufika pale nikapata watu hawanijui, nilifanya kazi mingi kwa dollar store, kufagia, nilikuwa nafanya kazi eighteen hours sababu lazima ushikanishe ndio upate ile pesa…  niliweza kusave na ivo ndio nilitengeneza my first million

Nilinunua taxi tatu, zilikuwa zinaitwa Jagz cabs, baadaye nikafungua garage.”