'Waliniita chokora na mtu asiyefaa,'Daddy Owen awashauri wakenya kuzungumza iwapo wana msongo wa mawazo

Muhtasari
  • Kwenye chapisho lake, anaelezea jinsi watu wengi wanaogopa kuongea ambayo hapo awali ilikuwa kesi yake
  • Daddy Owen awashauri wakenya kuzungumza iwapo wana msongo wa mawazo
Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN

Daddy Owen, ni mmoja wa watu mashuhuri wa Kenya ambao wamekuwa wakiwashangaza mashabiki wao kila siku kwa talanta za kipekee pamoja na ubunifu.

Anasimama miongoni mwa wasanii bora wa Injili nchini Kenya.

Daddy Owen ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuendelea na somo lake kuhusu afya ya akili aliloanza jana.

Kwenye chapisho lake, anaelezea jinsi watu wengi wanaogopa kuongea ambayo hapo awali ilikuwa kesi yake.

Daddy Owen anaendelea kueleza jinsi watu walivyokuwa wakimtaja kwa majina licha yake kuwa mtu mashuhuri.

" Jana baada ya kueleza kuhusu msongo wa mawazo na na afya ya akili nilipata mrejesho, na moja ya hoja kuu ni kwamba watu wanaogopa kuongea kwa sababu mtu atawasengenya baada ya kufunguka.. wacha ni waambie haya nilipitia hayo yote!

Watu niliokuwa nawaamini waliniita majina mvivu, dhaifu, asiyefaa, aliyechanganyikiwa, mwoga, chokora..!! nakadhalika!

Marafiki wengine walikuwa wakinijadili hata kwenye vikundi vya WhatsApp! Napigiwa simu usiku kwamba kuna mtu ninayemuamini yuko mahali fulani anajadili kunihusu jinsi nilivyo hoi!!!

Kumbuka mimi ni mtu mashuhuri wakati haya yote yanasemwa.. lakini unajua nini?? Namtumikia MUNGU ALIYE HAI!! Hatua nilizopiga kwa mwaka mmoja tu na nilizopata (siwezi kuanza kuziandika hapa ili mtu afikiri ninajisifu) ni ajabu tu! Waliniongelea lakini ili iweje!! Bado nilishikilia kichwa changu juu na kuchochewa na mazungumzo hasi kufikia haya yote!!" lisema Owen.

Baadaye anaonyesha maelezo ya jinsi alivyoyashinda yote, miongoni mwao maombi na kuzungumza.

"Katika kitabu changu kijacho nimetoa maelezo yote jinsi nilivyoshinda. 1. MAOMBI 2. MFUMO MZURI WA MSAADA 3. USHAURI (MCHUNGAJI NA MTAALAM) 4. KUFANYA KILE UNACHOPENDA 5. ONGEA! Orodha ni ndefu lakini hizi ni zingine ambazo zilinifanyia kazi."

Haya yanajiri baada ya mcheza Santuri kujiua, kutokana na madai alikuwa na shida ya afya ya akili.