Sababu kwa nini wachungaji wengi wanalala na wanawake walioolewa katika kanisani

Muhtasari
  • Sababu kwa nini wachungaji wengi wanalala na wanawake walioolewa katika kanisani
Picha ya watu wanaoshiriki katika tedno la ndoa
Picha ya watu wanaoshiriki katika tedno la ndoa
Image: MALAYALAMEMAGAZINE.COM

Tumesikia kuhusu kesi kadhaa ambazo ni zaidi ya moja ambayo wachungaji wanalala na kubarkiwa na watoto na washirika wao licha yao kuwa kwenye ndoa na wenzi wao.

Je! Umejiuliza kwa nini kesi zinazidi kuongezeka kwa kila kuchao?

Chini ni baadhi ya sababu kwa nini wachungaji wengi wamekuwa wakitekeleza mambo hayo, licha yao kuwa wachungaji.

1.Mchungaji hana maadili.

Hii ni sababu ya kwanza kabisa na kubwa. Hakuna njia mchungaji mwenye maadili mema ataenda kulala na waumini wa kike au hata mke wa mtu.

Je, mchungaji anawezaje kuhubiri dhidi ya uzinzi na usherati kisha aendelee kufanya uovu huo pamoja na washarika wake mwenyewe? Nafsi safi isiyo na maadili.

2.Mazingira ya majaribu wakati wa mashauri ya faragha na vipindi vya maombi

Baadhi ya wanawake wakiwemo wanawake walio kwenye ndoa humtembelea mchungaji kwa vikao vya ushauri na maombi maalum kuhusiana na masuala ya kibinafsi.

Huku baadhi yao wakienda kwenye mazingira hayo na mavazi ya aibu na ya kujaribu mchungajoo, kumbuka pia mchungaji ni mwanadamu na ana hisia kama mwanadamu

3.Wanawake wanamtongoza

Sasa niambie, upo hapo na maadili yako mema na kujitolea kuwa safi lakini hawa binti za Yezebeli wanaonekana wamevalia kwa ushawishi kanisani, wanakaa viti vya mbele na wanakutendea vizuri sana.

Hata kama yeye ni mchungaji, usisahau yeye pia ni mwanamume na wanaume wanavutiwa na kuona.

Je nani wa kulaumiwa katika mazingira haya, ambayo wengi wamekata tamaa na kusema kwamba hawataudhuria kanisa kwa sababu ya vitendo tofauti.