logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Cardi B ashinda kesi dhidi ya Mwanablogu Tasha K

Cardi alimstaki Tasha K  kwa kuweka video ambayo alikuwa anaeleza kuwa Cardi B ni Kahaba ambaye alijihusisha na dawa za kulevya na aliambukizana magonjwa ya zinaa

image

Burudani25 January 2022 - 12:05

Muhtasari


  • •Ameshinda kesi aliyopeleka kortini mwaka wa 2019  dhidi ya Tasha  K,ambapo alidai mwanablogu huyo alitunga uwongo kumhusu kwenye mtandao wake wa  kijamii
  • •Cardi alimstaki Tasha K  kwa kuweka video ambayo alikuwa anaeleza kuwa Cardi B ni Kahaba ambaye alijihusisha na dawa za kulevya na aliambukizana magonjwa ya zinaa
  • •Hakimu alisema fidia zozote za adhabu ambazo Tasha anaweza kumdai Cardi zitaamuliwa katika kesi ya baadaye.
Cardi B

Rapa wa Marekani ameshinda kesi aliyopeleka kortini mwaka wa 2019  dhidi ya Tasha  K,ambapo alidai mwanablogu huyo alitunga madai kumhusu kwenye mtandao wake wa  kijamii.

Cardi B alimshtaki Tasha K  kwa kuweka video ambayo alikuwa anaeleza kuwa Cardi B ni Kahaba ambaye alijihusisha na dawa za kulevya na aliambukizana magonjwa ya zinaa.

Kulingana na Mtandao wa TMZ, Cardi alidai mwanablogu huyo alitunga uwongo mbaya kumhusu jambo ambalo  halikuwa rahisi kujitetea ila kupeleka mahakamani.

Baada ya kusikizwa kwa wiki moja, makahakama imempata Tasha K na hatia ya makosa matatu  na kuamuru kulipa Cardi  pauni milioni 1.25 kama uharibifu wa jumla na pauni 250,000 kwa gharama za matibabu.

 

Kabla Cardi kuwasilishe kesi hiyo kortini mwaka wa 2019 alikuwa amepigia simu Tasha na kumtaka aondoe video hio kwenye ukurasa wake lakini alidinda kufanya hivyo.

Hakimu alisema fidia zote za adhabu ambazo Tasha anaweza kumdai Cardi zitaamuliwa katika kesi ya baadaye.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved